Hifadhi ya Mkomazi
Mandhari
Hifadhi ya Mkomazi ipo katika mikoa miwili ambayo ni Kilimanjaro na Tanga, ndani ya wilaya za Same na Lushoto nchini Tanzania.
Hifadhi ya Mkomazi ilianzishwa mnamo mwaka 1951 kama Pori la Akiba lililotengwa kutoka katika Pori kubwa la Akiba la Ruvu.
Hifadhi hii ina ukubwa wa kilometa za mraba 3245 (kilometa za mraba 2010.4 ni Mkomazi na kilometa za mraba 1224.1 ni Umba).
Pori hili lilipendekezwa kuwa hifadhi ya taifa kwa misingi ya kunusuru maeneo na rasilimali zilizomo kutokana na matumizi yasiyoendana na uhifadhi kwa ajili ya kizazi cha leo na kijacho.
Katika hifadhi hii kuna wanyama na ndege wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na mbwa pori na vifaru weusi walioingizwa kutoka nchi ya Afrika Kusini.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Orodha ya milima ya Tanzania
- Mbuga za Taifa la Tanzania
- Orodha ya milima ya mkoa wa Kilimanjaro
- Orodha ya milima ya mkoa wa Tanga
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Majarida ya hifadhi za Taifa Tanzania
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- TANAPA
- Utalii wa Tanzania Archived 13 Januari 2010 at the Wayback Machine.
- Maliasili za Tanzania
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hifadhi ya Mkomazi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |